Zum Inhalt springen

Auswahl der Sprachversion
Logo der LVR-Luise-Leven-Schule in Krefeld
Schüler der LVR-Luise-Leven-Schule spielen freudig

Kiswahili

Taarifa muhimu kuhusu huduma zetu za ushauri

Katika kituo cha ushauri tunajibu maswali kuhusu watoto wachanga, watoto au vijana wenye ulemavu wa kusikia. Tunawashauri wazazi, walimu wa aina zote za shule, wataalamu kutoka shule ya chekechea au elimu ya nyumbani, matabibu au wataalamu wengine wanaosaidia na kuwalea watoto kwa aina mbali mbali. Tunakushauri na kukepea mawaidha kuhusu aina mbali mbali za usaidizi. Kuna msaada mwingi na njia nyingi za kusaidia kila mtu anayehusika. Kwa pamoja tunatafuta masuluhisho bora zaidi kwako na kwa mtoto wako.

Ofa zetu za ushauri hazilipishwi.
Wasiliana nasi!

Je, ninaweza kufanya mashauriano vipi ikiwa sielewi Kijerumani?:

Tunaweza kujaribu kuagiza usaidizi wa mtafsiri kupitia serikali ya jiji la Krefeld. Tunamtafuta mtu anayezungumza lugha yako na Kijerumani vizuri.
Hii haimaanishi yakwamba yeye ni mkalimani.
Kwa sababu hii, hatuwezi gharamia ukamilifu. Huduma hii hailipishwi.
Tafadhali wasiliana nasi ikiwa huwezi kufanya mashauriano kwa Kijerumani.

Kanuni ya Corona:

Zingatia:

Katika waakati huu wa janga la corona, kuna njia mbili za kushauriana nasi:

Chaguo la kwanza: Unaleta uthibitisho wa kipimo hasi cha corona kutoka siku hiyo hiyo. Kisha tunaweza kukutana ana kwa ana kwenye kituo cha ushauri.

au:

Chaguo la pili: Tunakutana kwenye Mtandao kupitia gumzo la video.
Unahitaji mtandao thabiti na Kifaa chochote cha mawasiliano kwa mfano (simu mahiri, kompyuta kibao, kompyuta ndogo). Kiungo cha mtandao (link) kitatumwa kwa anwani yako ya barua pepe.

(Tafadhali kumbuka kuwa hatuwezi kuhakikisha tafsiri sahihi.)